Thursday, 31 January 2013

BUNGENI : Mwigulu Nchemba Afunguka

Leo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu, katika maswali aliyoulizwa, swala la  uzoefu wa kazi anayoomba mtu ni mojawapo ya maswali aliyoulizwa Wziri mkuu na Mh. Mwigulu Lameck Mchemba(MB). Mwigulu alimtaka waziri mkuu kwa niaba ya serikali atoe tamko la kufutwa kwa kigezo cha uzoefu wa kazi husika, kwana vijana wengi wanaohitimu vyouni hawana uzoefu kwani ndiyo inakuwa mara yao ya kwanza kuomba kazi. Hata hivyo hakuna chuo mahali popote duniani kinachofundisha uzoefu wa kazi, Mh. Mwigulu aliongeza.
Katika majibu yake Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda maarufu mtoto wa mkulima, alisema ni kweli wamekuwa wakifanya hivyo wanapotangaza baadhi ya kazi na si kazi zote kigezo cha uzoefu kilichukuliwa mojawapo ya vigezo. Hata hivyo pamoja na majibu mengine aliyotoa amesema bado sekta ya Uwalimu na Afya zina upungufu mwingi wa watumishi mbali na serikali kujiandaa kuajiri walimu zaidi ya elfu ishirini na tano mwaka huu.

Pamoja na swala la ajira kuibuka bungeni leo, maswala ya gesi mtwara hayakubaki nyuma. Kwani Mh. waziri mkuu alitoa taarifa fupi bungeni juu ya ziara yake mtwara kusuluisha mgogoro uliyofukuta hivi karibuni juu ya gesi. Na Mh. kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni katika maswali aliyomwuliza waziri mkuu, mojawapo alimtaka waziri mkuu akili kuwa serikali yake ni sikivu pindi inaposukumwa.
Waziri mkuu aliitimisha kipindi chake kwa kuwashukuru wanamtwara pamoja na kuwapa pole waliyofikwa na dhahama la gesi Mtwara wakiwemo wabunge viongozi wa serikali, na chama (CCM) wa Mtwara.
Nakumegea kiduchu, zaidi tembelea tovuti ya bunge.
Ni mimi the Blogger G.

Waheshimiwa Wabunge wakiwa moja ya vikao Bungeni. Picha na Tovuti ya Bunge

4 comments:

Mathematics Teku said...

Mwalim nyerere alisema huwezi kuwa kiongozi kama sehemu moja ya nchi mambo yanakwenda hovyo kama mtwara ilivyo,hivyo mizengo kama ni mzalendo na wenzake wawajibike Habonga Jopha

Mathematics Teku said...

gjfffgggggg by km

Mathematics Teku said...

Kaka hizo ni siasa za chama tawala ili waendelee kubaki madarakani, tuachane nao, tuangalie mambo ya tensor analysis tu.by Watson Sikitu.

Mathematics Teku said...

Corruption in Africa and other part of the world. In Europe there is corruption also in Africa there corruption too.Europe the contract of building a road may be awarded to the son of president also in Africa the road can be awarded to the son of president,now the difference is in Europe the road will be built but in africa especially in Tanzania will not.Tutashindana na wazungu hawa wanaotaka kuhamia MTWARA?>>>>>>MWENE MWAMLIMA BM

Post a Comment