Wednesday 6 February 2013

Elimu Tanzania na Ubora Wake

Ni miaka kadha wa kadha nimekuwa nikijitahidi kutaka kujua mfumo wa elimu Tanzania umejengeka katika misingi ipi. nidhahili kuwa maendeleo ya jamii yoyote au mtu binafisi inaamliwa na kiwango cha maarifa aliyonayo. nikafikiri pia njia muhimu na ya msingi katika kupata maarifa ni kupitia kusoma ama kujielimisha.
Katika bunge linaloendelea la kumi la Jamhuri Mh. Mbatia(MB) kawasilisha hoja binafisi juu ya mfumo wa elimu tanzania. Pamoja na mambo mengine Mbatia anataka kujua kama nchi ina mtaala wa elimu na kama hupo apatiwe.

Nina maswali kadha katika utafiti wangu( Elimu Tanzania).Haya ni baadhi ya maswali yangu, Naomba kujibiwa:
1. Nini tofauti kati ya Mtaala (Curriculum) na Silabasi (Sylabus)?
2. Tokea uhuru Tanzania imeishakuwa na mitaala mingapi, tofauti yake na ipi?

No comments:

Post a Comment